Yapo mambo mengi/vitu vingi vya kuzingatia wakati wa ununuaji wa simu, lakini hapa nimekuletea machache ya muhimu ambayo yanaweza kuwa ni muongozo katika hatua ya ununuzi wa kifaa hicho cha mawasiliano.
- Mazingira/Eneo Ulipo
- Mahitaji/Ulazima wa Aina ya Simu
- Uwezo wa Simu Husika/Vilivyomo Uwezo wa simu kukaa na betri (japo inategemea na matumizi yako) Uwezo wa simu kuhifadhi vitu (storage capacitykupokea; kwa mfano intaneti (uwezo tofauti wa kasi ya mawimbi ya mtandao, 2G, 3G, 4G au G4 LTE) na mawasiliano ya kawaida ya kupiga simu na utumaji wa ujumbe. Kiwango cha uhifadhi wa ujumbe unaopokea kutoka kwa wanaokutumia (baadhi ya simu huwa na kiwango cha chini ya jumbe 100 katika kisanduku cha kuhifadhia – inbox, hivyo kumlazimu mtumiaji kufuta baadhi ya jumbe hata kama ni za muhimu ili kuruhusu ujumbe mwingine kuingia)
- Mahitaji mahsusi ya mtumiaji kama vile; radio (inayotumia antena au ya bila antena), muziki wa simu (mp3 player), uwezo wa kamera pamoja na ubora wa picha zinazopigwa, mwanga wa simu (brightness), ukubwa wa kioo na ubora wake wa uoneshaji wa picha/video – (display quality), pamoja na uwezo wa simu kukubali kihifadhi cha ziada (MicroSD/Memory Card)
- Gharama – kwa maana ya kuzingatia uwezo wako wa kiuchumi. Hili pia linasimama katika upande wa vifaa vya simu pindi vinapopata matatizo kwa maana ya upatikanaji na ununuzi wake.
- Aina ya muundo wa uendeshaji wa simu (Operating Systems – OS, kwa upande wa “smartphones” – kama vile; iPhones, Windows, Android, Blackberry n.k)
- Mahitaji ya kitaalamu, hususani kwa upande wa “smartphones” ambavyo ni; RAM, Processor, usalama wa ufungaji simu (lock).
Kisibi Isaya - Mwandishi wa Makal |
Chapisho hili liliruka hewani kupitia kituo cha matangazo ya redio cha Radio Free Africa - R.F.A ya jijini Mwanza (Inayosikika nchini kote) katika kipindi cha Techno Kweli - Ubunifu na Maarifa tarehe 10/Novemba/2015
Post A Comment: