VIASHIRIA VYA KUTAMBUA KWAMBA BETRI IMEFIKA MWISHO WA MATUMIZI NA INAHITAJI KUBADILISHWA.



Viashiria
·         Kuvimba kwa betri
·         Kwisha Mara kwa Mara
·         Kujichaji bila kuchomeka kwenye chaji
·         Kuwahi kuisha chaji licha ya matumizi madogo  ya kiwango cha umeme.
CHANZO
·         Aina ya betri (mchanganyiko wa material yaliyotumika kutengenezea)
·         Kwa kiwango gani betri haiko katika moto (kuchajiwa), baadhi ya betri hushauliwa kuwa, ziondolewe katika chaji baada ya kujaa kwa 100% lakini pia kuna baadhi ya betri mfano; Lead Acid na Lithium-Ion/Li-Ion inashauriwa kuwa  usizitoe kwenye chaji mara kwa mara kabla ya kujaa kwani husababisha kiwango chake cha uhifadhi wa chaji kishuke hata kama imejaa kwa 100%
·         Huduma ya betri (adherence to battery service) baadhi ya betri hazihitaji kufanyiwa huduma au marekebisho lakini pia kuna baadhi ambazo huitaji, endapo ikitokea aina ya betri unayotumia ina uhitaji wa huduma hiyo, ni vema kufanya hivyo ili kuweka uwiano wa kiwango chake cha matumizi.
·         Joto la eneo – joto ni moja kati ya vitu ambavyo hudumaza kwa kiasi kikubwa sana viafaa vingi vya umeme, ikiwemo betri
-
Kuna mengi sana unaweza ukawa umesikia kuhusu njia nzuri za kuchaji simu yako. Pia utakuwa umesikia kuhusu vitu ambavyo hutakiwi kufanya ukiwa unachaji simu.
Je yana ukweli wowote?
Leo tutakuelezea kwa uchache na kwa ukweli mambo muhimu kuhusu kuchaji kwa simu na usalama wa betri za simu wakati tukiwa tunazichaji.
·         Kutumia chaja ambazo si za makampuni ya simu zinaua simu
Hapana, hakuna ukweli kabisa katika hili ila ukweli ni kwamba usitumie chaja za ubora mbovu. Chaja feki si chaja zote ambazo hazitengenezwi na kampuni husika ya simu bali ni chaja ambazo zipo chini ya kiwango. Na hizi utazigundua kupitia bei zake, usikubali kumiliki simu ya gharama halafu ukawa mbahili katika kununua chaja za uhakika kisa bei zake.
Cha kufanya soma kuhusu kiwango na ubora wa chaja inayofaa kwenye simu yako kabla ya kununua chaja isiyokuja na simu yako.
·         Usitumie simu yako wakati unaichaji
Si kweli, ni kweli zamani sana, kwa sasa teknolojia inayotumika kwenye chaja na simu ni salama kabisa. Cha kuhakikisha ni kwamba unatumia chaja zilizo na kiwango/ubora wa uhakika (original/quality). Kumbuka hapa haimaanishi ni kwamba lazima iwe ni yenye lebo/nembo ya kampuni husika bali hili ni suala la kuwa ni chaja yenye ubora wa uhakika.
·         Usizime simu yako kamwe!
Si kweli! Unashauriwa kuzima simu yake angalau ata mara moja kwa wiki kwa angalau lisaa. Simu kama vifaa vingine vyote vya umeme ni muhimu kupata muda wa kupumzishwa. Na jambo hili ndio linaboresha zaidi uhai wa simu yako.
·         Kuchaji simu usiku kutaiua/haribu
Usisikilize hii… si kweli! labda kama unatumia simu iliyotengenezwa miaka ya 1980 Teknolojia imekua sana, fahamu ya kwamba simu zote za siku hizi zitaacha kutumia umeme pale simu yako itakapochaji hadi asilimia 100! Itaacha kuchaji! Hakuna madhara! Ila hii haimaanisha ndio uiache kwa zaidi ya masaa 15! na pia kuhakikisha unaichaji sehemu inayopata hewa.
·         Subiri hadi chaji iwe chini kabisa au imeisha ndio uchaji
Hili sio kweli! Ukweli ni kwamba kuchaji mara kwa mara ndio kunasaidia zaidi kuongeza maisha ya betri yako. Kumbuka kuchaji mara kwa mara si kila baada ya dakika 5, bali ni kwamba usisubiri chaji iwe chini ndio uchaji, na si lazima ukiweka kwenye chaji usiitoe hadi imejaa, na inashauriwa kitaalamu kuwa angalau simu yako ikiwa chini ya asilimia hamsini (50%) uichaji.

Kuna aina kuu mbili za mabetri yanatumika kwa sasa
Kuna mabetri yanayotumia teknolojia ya Lithium-Ion (Li-ion) na Lithium-Ion-Polymer (Li-ion Polymer/Lithium Polymer). Kuna teknolojia nyingi zilizokuwepo zamani ila kwa sasa hizi ndio zinazotumika zaidi. Na zinatumika kutokana na ubora wake. Lithium-Ion (Li-ion) zinatumika zaidi katika simu nyingi zaidi wakati betri za Lithium-Ion-Polymer zinatumika zaidi katika kompyuta mpakato (laptop) na baadhi ya simu pia. Lithium-Ion-Polymer ndio teknolojia bora zaidi na salama zaid, Lithium-Ion ni salama pia kwa kiwango kikubwa sana ila Lithium-ion-polymer ni zenye ubora zaidi na hii inaweza kuwa ni sababu kubwa zinatumika kwenye laptop nyingi tayari.
Teknolojia hizi zimefanya ulipukaji ovyo wa mabetri ya simu kuwa mgumu sana kuliko unavyofikiri.


Makala hii   iliruka katika kituo cha matangazo ya redio - Radio Free Africa, tarehe 7/Juni/2016 kuanzia saa 3:15 usiku hadi 4:00 usiku.
Issack Msumba na Kisibi Isaya

#KicbjamiiTanzania Kwa mawasiliano zaidi (contacts): kisibilive@gmail.com or kicbjamii@yahoo.com Skype - live:kicbjamii Twitter/Instagram - @kicbjamii
Axact

Post A Comment: