Katika ulimwengu wa sasa wa ubunifu pamoja na maarifa mengi ya kibinadamu, kumekuwa na maneno mengi ya kiteknolojia pamoja na vifaa vinavyoendana na maneno hayo. Mojawapo ya maneno ni PIXEL na mara nyingi tumekuwa tukilisikia neno hili pamoja na kulizungumza aghalabu katika masuala ya kimawasiliano na habari.


Pixel (pel) ni nini?
Neno pixel linatokana na kufupishwa kwa maneno ya kiingereza “Picture Element” ambapo kwa Kiswahili tunaweza kusema ni sehemu unganishi ya picha na zinapokuwa nyingi na kutengeneza umbo la tunasema ni picha.

Historia ya pixels katika teknolojia ya picha.
Inaelezwa kuwa mnamo mwaka 1839 kulipokuwa na majaribio pamoja na picha za kibiashara ndipo kulipokuanza kutumika kwa pixel japo haijathibitishwa sana kwani aliyekuwa muigizaji wa kidachi na muongozaji wa video/michezo ya maigizo jukwaani, Willy Van Hemert (Machi 29,1912 kufariki Juni 26, 1993) anaelezea kuwa matumizi ya pixels yalikuja baadaye kabisa hasa baada ya ugunduzi wa televisheni za rangi katika miaka ya 1950 na ndipo dunia iliposogea sana katika mapinduzi makubwa kimaendeleo ya teknolojia ya matumizi ya pixels.
—–
Megapixel ni nini?
Katika miaka ya hivi karibuni, neno megapixel limeshika kasi sana, hii kutokana na mabadiliko ya kimfumo wa maisha hususani katika suala la mawasiliano pamoja na mfumo wa upashanaji habari na si adhimu sasa kusikia watu wakizungumza kuhusu neno hili.
Baada ya kufahamu kwa undani kuhusu neo pixel tufahamu pia kuhusu neno “mega”

Mega – kwa mujibu wa kamusi mbalimbali pamoja na tafsiri za lugha neno “mega” hutumika kuelezea kiwango cha ukubwa kuhusu kitu/jambo Fulani, na mara nyingi tumekuwa tukisikia hususani katika masuala ya muziki kukiwa na neno Mega Music System ama katika upande wa kompyuta hususani kwenye suala la uhifadhi wa taarifa, neno megabytes (MB) limekuwa likitumika sana… (maelezo kwa ufupi kuhusu mega music system/megabytes kwa mrandano na neno mega katika kamera)
Kwa pamoja ukichukua maneno hayo ndipo tunapata neno “MegaPixel” na tafsiri yake imejikita zaidi katika maelezo hayo lakini kwa kifupi tu ni kuwa, Megapixel – ni kipimo/kiwango cha ubora wa picha inayochukuliwa na kamera ya kisasa (digital camera), ambapo tunaweza kusema ya kuwa megapixel 1 ni sawa na pixels milioni moja (1,000,000)
Kwa mfano kama kamera ya simu inaweza kuchukua ukubwa wa picha kwa kiwango cha ukubwa wa 640 kwa 480 ambapo ukizidisha hapo tunapata laki tatu elfu saba na mia mbili (307,200) hivyo tunasema kuwa kamera hiyo ina uwezo wa megapixel 3.

Neno megapixel tunaweza pia kulitamka kwa kifupi kama “MP” na ndivyo hata ukiangalia katika kamera nyingi za simu/za digitali wameandika kwa ufupisho huo.
Kitambo kidogo ilizoeleka kuwa megapixel nyingi za kamera ya simu ni 1.3MP, 2MP, 3.2MP na 5MP lakini kutokana na mabadiliko ya sasa ya kiushandani katika teknolojia ya mawasiliano ya simu na mahitaji ya wakati (hususani uwepo wa mitandao ya kijamii) megapixel za kamera nyingi zimeboreshwa kwa kiwango cha juu kuweza kufikia megapixels 38 hadi 41 kwa simu za kisasa (smartphones) na mfano mmoja wa simu yenye kiwango hiki ni Nokia Lumia 1020.
Zingine zenye kiwango cha juu lakini chini ya 38 hadi 41 ni pamoja na;
  • Apple iPhone 5, 5c, 5s    3,264 x 2,448          8MP
  • Samsung Galaxy S4       4,128 x 3,096          13MP

Uchambuzi/Makala hii ililuka katika kituo cha matangazo cha Radio Free Africa (R.F.A) 13/Oktoba/2015.
Endelea kufuatilia machapisho mbalimbali nitakayokuwa nikuletea hapa.
Na, Kisibi Isaya
Axact

Post A Comment: