UTANGULIZI
Simu nyingi pamoja na baadhi ya vifaa vya umeme vinatumia betri ili kuzalisha umeme unaotumika kwaajili ya matumizi ya vifaa hivyo, lakini kumekuwa na changamoto kubwa sana katika suala la uimara wa betri.



HUTOKEAJE?
Kutokana na betri nyingi za simu kuwa nyembamba, hivyo kuwa vigumu kwa upatikanaji wa nafasi ya kutosha ya utenganishaji wa sehemu hasi na chanya hivyo basi hutumika kitenganisho kidogo sana (membrane [separator is a permeable membrane placed between a battery's anode and cathode. The main function of a separator is to keep the two electrodes apart to prevent electrical short circuits while also allowing the transport of ionic charge carriers that are needed to close the circuit during the passage of current in an electrochemical cell.[1] - Wikipedia) katika sehemu hizo ili kuruhusu betri kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.


Kama kitu chochote kikiingia / kuwekwa kati ya hivi vitu viwili (mfano ni uunganishaji wa betri kwenye chaji kwa kutumia sarafu) huweza kusababisha matatizo sana sana kama betri haijatengenezwa kwa viwango vinayotakiwa.


Chanzo kikubwa cha betri nyingi kulipuka ni matokeo ya hali au mchakato uitwao THERMAL RUNWAY na hii husababishwa na ongezeko la halijoto (temperature) katika namna ambavyo joto hupanda (hot) hivyo kusababisha mlipuko kutokana na msongamano wa hali ya matokeo chanya ya umeme.

KUEPUKANA NA KULIPUKA KWA BETRI
  • Tumia betri halisi kutoka kwa mtengenezaji au zinazotambulika na zenye viwango vinavyoruhusiwa kwa matumizi ya kifaa chako (simu, laptop n,k) kwani baadhi wamekuwa wakinunua betri za bei rahisi sana na zisizokidhi viwango.
  • usiache simu yake kwenye eneo lenye joto sana, haswa wakati wa kuichaji betri, kwani joto jingi huweza kuathiri mfumo wa umeme wa betri husika na simu yenyewe.
  • Endapo unachaji simu yako au unaitumia kwa matumizi yanayoifanya iwe katika hali ya joto la juu hakikisha simu yako iko huru (kwa maana ya kuitoa kwenye kasha/cover lake au kutokuiegemeza sehemu yenye kushabarabu joto)
  • Japo inaweza kuonekana kama ni jambo la kushangaza kidogo, lakini kama utaweza, inashauriwa kuchaji simu yako pindi tu betri yake chaji inapofikia angalau kiwango cha asilimia 50 ni kitu kizuri. Betri za aina ya Li-ion haziathiriwa sana na masuala ya uwezo wa kumbukumbu ya simu (memory issues) kama betri nyinginezo ingawaje zinaweza kuharibika endapo kama itawekwa kwenye kifaa chenye umeme mdogo sana.
  • Inashauriwa kila baada ya miezi 36 (kwa betri za lithium-iion /  li-ion) zibadirishwe (tumia betri sahihi) au japo haishauliwi sana, mtumiaji ajitahidi katika matumizi yake ya simu asisababishe mikwaruzano pamoja na muingiliano wa pande hasi na chanya za betri.
MAKALA HII ILIRUKA HEWANI MOJA KWA MOJA (LIVE) kupitia
RADIO FREE AFRICA (RFA)
TEKNOKWELI - Ubunifu na Maarifa | 01/Machi/2016
Issack Msumba & Kisibi Isaya
________________
Axact

Post A Comment: